K.I.B.A. K.I.B.A. -- Klubo Internacia de Bao-Amantoj
New! Usisahau kusajili kituo cha video ya Bao kwenye YouTube.

Mwongozo - 2


Jinsi ya kucheza bao kwa njia ya tovuti hii

ANGALIA: tovuti inabadilika mara kwa mara, kwa picha hizi za kurasa zinaweza kuwa tofauti.

ZINGATIA: Tunza namba yako ya siri!

1) Tembelea kwa www.kibao.org

2) Bonyeza Ingia

3) (Kama umeshasajili rukia kwa hatua 5) Hamisha kipanya mpaka utasoma juu ya shimo la mraba *** UJISAJILI ***' ukabonyeza

4) Jaza fomu na utunze Lakabu/Nuira na Namba ya siri. Utapata baruapepe na unatakiwa kuthibitisha usajili wako.

5) Hamisha kipanya mpaka utasoma juu ya shimo la mraba *** UKURASA BINAFSI ***' ukabonyeza

6) Utapata ukurasa wako. Wakati wa kwanza ukurasa huu utakuwa wazi, kwa hiyo unatakiwa kumwalika mchezaji fulani ili acheze nawe. Kwa hiyo, bonyeza juu ya alika upande wa kushoto wa ukurasa.

7) Utaona orodha ya wachezaji (Wanaokuwa wanacheza). Chagua mchezaji mmoja (kama wewe bado u mwanafunzi unashauriwa kuchagua mkufunzi!).

Baadaye inabidi usubiri baruapepe kutoka mchezaji uliomchagua. Utamwona mchezaji huyu katika Michezo huria ya ukurasa wako (taz. picha ya hatua 6) na bonyeza Cheza utakapotaka kucheza.

7a) Utapata ukurasa unaofanana na ufuatao

Ukibonyeza mchoro wa juu upande wa kushoto wa ukurasa huu

utapata ukurasa unaofanana na ufuatao

Kushoto unaona mchoro wa Bao. Mashimo yako ni ya chini, hata kama ukiwa kaskazini, kwa sababu ni zamu yako ya kucheza:

8) chagua shimo unamotaka kutia kete yako, na angalia herufi inayoendelea na shimo hii. Kwa mfano shimo lenye kete 11 lina herufi A. Huo ndio mstari wa shimo. Sasa bonyeza mshale chini ya Herufi ya mstari ili uone herufi ya shimo ulilochagua. Kwa lile shimo lenye kete 11, inakubidi uchague Ndani A/a

9) sasa tazama namba ya shimo ulilochagua. Namba hii inakaa chini. Namba hii ni namba ya safu ya shimo. Bonyeza mshale unaoona chini ya Safu na chagua namba ya shimo. Kwa mfano ukiwa umechagua shimo lenye kete 11 lazima uchague namba 5.

10) sasa chagua mwelekeo wa mzunguko wako kwa kubonyeza mshale unaoona chini ya neno Mwelekeo

11) amua ukitaka kucheza nyumba yako kwa kubonyeza Hapana au Ndiyo karibu na maneno 'Utacheza nyumba yako ikiwezekana?'

12) hatimaye bonyeza Tumia

13) ukurasa ufuatao utadhabitisha mzunguko wako na utakuonyesha matokeo ya mzunguko huu. Kwa mfano huu mchezaji alichagua A7<+*

14) Bonyeza Rekebisha ukitaka kubadilisha mzunguko wako, hali kadhalika bonyeza Tumia ukitaka kutumia mzunguko wako kwa mshindani wako atakayepata baruapepe yenye yanayofuata:

1: A6<* a5<;
2: A3> a5>;
3: A8< a7<*;
4: A5> a6>;
5: A6<* a6>;
6: A7<+*


Saleh: 17
b  0   0   0   0   0   0   0   0
a  1   2   4  10   0   0   0   0
---------------------------------
A  0   0   0   0  12   1   0   1
B  0   0   0   0   0   0   0   0
Nino: 17



Nino
nino@xxxxxxx.yy


http://www.kibao.org

yaani:


Sasa aliyepata baruapepe hii anapata zamu ya kucheza kwa kufuata maelezo ya hapa juu.

Ukitaka maelezo zaidi tafadhali utuandikie.

ZINGATIA: Tunza namba yako ya siri!

© Nino Vessella (w3.css), 2008 (×)