Jinsi ya kucheza bao kwa njia ya baruapepe
Ukurasa huu unawahusu watu wote ambao hawajajua kwamba inawezekana kucheza
Bao kwa njia ya barua na pengine hawajawahi kusikia chochote kuhusu uwezekano
wa kuandika mchezo.
[Baadaye soma
Jinsi ya kucheza bao kwa njia ya tovuti hii]
Inayofuata ni picha ya Bao:
Tunaweza kuchora bao hili hivi:
Sasa
tukae kwenye bao.
Wewe
ukae kaskazini
Mimi
nikae kusini
Kila mstari wa mashimo una jina lake.
Mistari yako ni
a -
b
Mistari yangu ni
A -
B
Hivi:
Hata mashimo yana majina:
Kwa hiyo mashimo yako ya mbele yanaitwa: a1 - a2 - a3 - a4 - a5 - a6 - a7 - a8
ambapo, mashimo yako ya nyuma yanaitwa: b1 - b2 - b3 - b4 - b5 - b6 - b7 - b8
Mashimo yangu ya mbele yanaitwa: A1 - A2 - A3 - A4 - A5 - A6 - A7 - A8
na
mashimo yangu ya nyuma yanaitwa: B1 - B2 - B3 - B4 - B5 - B6 - B7 - B8
kaskazini = WEWE
b
b8
b7
b6
b5
b4
b3
b2
b1
a
a8
a7
a6
a5
a4
a3
a2
a1
A
A1
A2
A3
A4
A5
A6
A7
A8
B
B1
B2
B3
B4
B5
B6
B7
B8
kusini = MIMI
Kwa hiyo nyumba yako inaitwa
a5, ambapo yangu inaitwa
A5 (Soma
Kanuni za kuandika mchezo wa bao kwa maelezo zaidi).
Sasa tunaweza kuanza mchezo.
Naanza mimi, kwa sababu mimi ni
kusini, kwa kucheza shimo
A6 kuelekea kushoto, yaani ninatia kete moja kwenye shimo la sita kuanzia kushoto nikachukua kete tatu nikazitia kwenye mashimo ya tano, nne na tatu.
Utajuaje nilifanya nini?
Nitakuandikia katika barua:
A6<, yaani naanza kutoka shimo la
6 la mstari
A nikaelekea kushoto ('<') (Soma
Kanuni za kuandika mchezo wa bao kwa maelezo zaidi).
Wewe utajua kwamba sasa hali ya bao ni hivi:
Wewe bila shaka utataka kuchukua kete yangu yaliyomo shimo
A4, na labda
utapenda kuitia kwenye shimo lako la kwanza kuanzia kulia, basi katika baruapepe utayonipelekea utaandikia:
a5> (Soma
Kanuni za kuandika mchezo wa bao kwa maelezo zaidi).
Hivi nitajua kwamba hali ya bao itakuwa hivi:
Ukitumia tovuti hii unaweza kucheza kwa urahisi zaidi kuliko kufuata mambo yanayotangulia.
Soma
Jinsi ya kucheza bao kwa njia ya tovuti hii
Sasa uko tayari kusoma kanuni za mashindano kwa njia
ya baruapepe!
Vile vile unaweza kumtafuta mchezaji binafsi na kucheza naye kwa njia ya baruapepe.